Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:31 am

NEWS: IFAHAM SAFU MPYA YA UTEUZI YA RAIS MAGUFULI BARAZA LA UWONGOZI

Dar es salaam: Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za uongozi uliotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo amemteua Mhe. Anjellah Kairuki kuwa Waziri wa Nchi, Osi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji ambapo kabla ya uteuzi huo Mhe. Kairuki alikuwa Waziri wa Madini. Katika mabadiliko hayo aliyekuwa naibu waziri wa madini Mhe. Doto Biteko ameteuliwa kuwa kuwa Waziri wa Madini ambapo sasa wizara hiyo itakuwa na naibu Waziri mmoja ambaye Mhe. Stanslaus Nyongo huku Mhandisi Joseph Nyamuhanga akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Osi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Aidha Dkt. Zainabu Chaula ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia afya huku Elius Mwakalinga akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ujenzi akitokea Wakala wa majengo ambapo alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala huo.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Dorothy Mwaluko kuwa Katibu Mkuu, Osi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji),Dkt. Dorothy Gwajima kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Afya),Dkt. Francis K. Michael kuwa Naibu Katibu Mkuu, Osi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mpoki Ulisubisya ameteuliwa kuwa Balozi na kituo chake cha kazi kitatangazwa hapo baadaaye. Prof. Faustin Kamuzora ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Bw. Athumani Diwani Msuya ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Uapisho wa viongozi hao utafanyika januari 9 mwaka huu Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameifuta nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi. Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa Bi. Immaculate Ngwalle ambaye amestaafu. Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amefanya uamuzi wa kufungua Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Cuba. Balozi wa Tanzania nchini Cuba atateuliwa baadaye.