- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDADI YA WATU YAFIKIA 276 WALIOFARIKI KWENYE SHAMBULIO LA BOMU SOMALIA
Mogadishu: Idadi ya watu imeendelea kuongezeka kwenye milipuko iliyotokea Mogadishu ambapo Takriban watu 276 wanaripotiwa kufariki Dunia . Mamia ya watu wengine wanaripotiwa kujeruhiwa. Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, siku mbili baada ya nchi yake kukumbwa na mauaji mabaya kabisa kuwahi kutokea tangu mwa mwaka 2007.
Lakini mpaka sasa hakuna kundi hata moja ambalo limejitokeza na kudai kuhusuka na mauaji hayo yaliyotokea kwenye eneo linalotembelewa na watu wengi katikati mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
Shambulio hili lilitokea saa chache baada ya Waziri wa Usalama wa raia nchini humo na Mkuu wa majeshi kujuzulu kwenye nafasi zao.
Katika shambulio la kwanza, bomu lilokuwa kwenye lori, lililipuka kwenye njia panda, iitwayo Kilomita-5, ambapo kuna ofisi za serikali, mahoteli na maduka, vyote viliporomoka katika mlipuko huo.
Saa mbili baadaye, bomu jengine lilikalipuka katika mtaa wa Medina.
Mlipuko huo ulitokea dakika chache tu baada ya lori lililoegeshwa na vilipuzi kulipuliwa karibu na
Baadhi ya mashahidi wanasema kuwa hoteli ya Safari ilianguka huku watu kadhaa wakidaiwa kukwama chini ya vifusi vyake, wakiongeza kuwa wanaamni kuwa watu wengi waliangamia katika mlipuko huo.