- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDADI YA WALIOFARIKI ZIWA VICTORIA UGANDA IMEFIKIA 30
Taarifa kutoka jeshi la Uwokozi la nchini Uganda zinadai kuwa Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuzama kwa boti katika Ziwa Victoria nchini Uganda, Jumamosi iliyopita, imefikia zaidi ya 30, wakati huu zoezi la kutafuta miili zaidi ikiendelea.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Zura Ganyana amesema kuwa hadi sasa watu walionusurika ni 27 huku zaidi ya 60 wakiwa bado hawajapatikana.
Boti hiyo inaelezwa kuzama umbali wa mita 150 kutoka ufukweni na Sababu za kuzama zinaelezwa kuwa huenda ni idadi kubwa ya watu na hali mbaya ya hewa katika Ziwa hilo.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesikitishwa na ajali hiyo. Ripoti za awali zinasema kuwa, boti hiyo haikuwa imesajiliwa na haikuwa na kibali maalum cha kufanya safara za maji.
Mauaji haya, yanakuja, miezi karibu miwili, baada ya watu zaidi ya 200 kupoteza maisha katka Ziwa hili nchini Tanzania.
Safari za maji katika Ziwa Victoria, zinaendelea kuwa hatari kutokana na uwezo mdogo wa kuwaokoa watu waliozama lakini pia bodi vibaya.