- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : ICC IMEPANGA KUCHUNGUZA JINAI ZINAZOFANYIKA NCHINI BURUNDI
ICC kuchunguza jinai zilizofanyika nchini Burundi
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa kibali cha kuanzishwa uchunguzi wa jinai na ukatili uliofanyika nchini Burundi licha ya nchi hiyo kujiondoa katika mkataba uliounda mahakama hiyo mwezi uliopita.
Taarifa iliyotolewa na ICC imesema majaji wa mahakama hiyo wameruhusu kuanzishwa uchunguzi kuhusu ukatili na jinai dhidi ya binadamu uliofanywa katika kipindi cha kati ya mwaka 2015 na 2017 dhidi ya raia wa Burundi ndani au nje ya nchi hiyo.
Jinai hizo ni pamoja na mauaji, ubakaji, ukatili na mateso vilivyoanza mwaka 2015 baada ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kugombea kiti hicho kwa muhula wa tatu mfululizo.
Taarifa ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imesema kuwa, inakadiriwa kwamba watu 1200 wameuawa, maelfu wameswekwa jela kinyume cha sheria, maelfu ya wengine wameteswa na mamia wametoweka.
Ripoti hiyo imesisitiza kuwa ukatili huo umewalazimisha watu zaidi ya laki nne kukimbia makazi yao katika kipindi cha kuanzisha mwaka 2015 hadi mwezi Meimwaka huu wa 2017.
Kibali cha kufanyika uchunguzi kuhusu jinai zilizofanyika huko Burundi kimetolewa baada ya Mwendesha Mashitaka wa ICC, Fatou Bensouda kusema kuwa, uchunguzi wake umepata ushahidi unaothibitisha kuwa polisi na askari usalama wa serikali ya Burundi walifanya mashambulizi ya makusudi dhidi ya raia. Bensouda ameongeza kuwa, mashambulizi hayo yalihusisha "vitendo vingi vya mauaji, vifungo, mateso, ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kingono, kupotezwa raia na kadhalika.
Msemaji wa serikali ya Burundi, Philippe Nzobonariba amesema kuwa Bujumbura haitashirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa sababu si mwanachama tena wa mahakama hiyo.