- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HUENDA RAIS KABILA AKARUDI MADARAKANI TENA
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Joseph Kabila anaondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi huu lakini hajaondowa uwezekano wa kutaka kurudi tena madarakani hapo baadae.
Kabila amezungumza na shirika la habari la Associated Press na kusema kwamba anataraji kuendelea na shughuli za kuzitatua changamoto nyingi katika nchi hiyo iliyoko kwenye eneo la Afrika ya Kati.
Kiongozi huyo wa Kongo pia amebaini kwamba amefanya kile alichoweza kwa faida ya Kongo tangu alipoingia madarakani mwaka 2001 baada ya kuuliwa baba yake Laurent Kabila.
Hata hivyo amesema bado kuna mengi ya kufanywa. Katika mazungumzo na shirika hilo la habari la AP amepuuza hofu za upinzani kwamba ataendelea kuitawala nchini hiyo kupitia mlango wa nyuma baada ya kuondoka madarakani ikiwa Emmanuel Ramazani Shadary anayemuunga mkono atachaguliwa rais katika uchaguzi huo wa desemba 23.Kabila amesema katiba ya Kongo inaweka wazi kwamba hakuna utaratibu kama huo unaoweza kufanyika.