- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA YANG'ARA YAANZISHA UPASUAJI WA MATUNDU MADOGO.
DOM: Hospital ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma, kwa mara ya kwanza imeanza kupima na kufanya upasuaji wa wagonjwa kwa kutumia matundu madogo kwa maradhi ya wanawake.
Aidha itaanza kufanya uchunguzi na upasuaji kwa kutumia teknolojia hiyo ya kisasa kwa magonjwa ya koo, masikio, pua na saratani ya utumbo mpana.
Akizungumza Julai 25 hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dk. Alphonce Chandika, amesema vyumba sita vya upasuaji vimeshaandaliwa kutoa huduma hiyo ya upasuaji ambayo inafanywa kwa kushirikiana na timu ya madaktari kutoka Marekani.
Amesema vifaa vya kisasa vilivyounganishwa na mfumo wa tiba mtandao utawawezesha madaktari kuwasiliana na wataalamu wenzao popote walipo na kutoa ushauri wa kitabibu wakati mgonjwa akiwa anafanyiwa upasuaji.
“Kipimo hichi kinachotumia teknolojia ya uchunguzi kwa njia ya matundu madogo kinawezesha kutoa jibu la uhakika zaidi na kufahamu tatizo halisi linalomsimbua mgonjwa.
“Kadhalika upasuaji wake hauusishi mgonjwa kupasuliwa sehemu kubwa, lakini pia mgonjwa kutopata maumivu makubwa na anachukua muda mfupi kupona,” amesisitiza.
Pia daktari huyo alieleza kuwa hospitali hiyo pia inafanya upasuaji wa mifupa kwenye goti pamoja na tezi dume.
“Upasuaji wa tezi dume tunaoufanya hatumpasui mgonjwa kupitia njia ya kibofu bali ataingizwa kifaa maalum kupitia njia ya mkojo, hivyo tunawahamasisha wanaume wenye umri kuanzia miaka 45 wajitokeze kufanyiwa uchunguzi,” ameeleza Dk huyo.
Hata hivyo DkChandika amesema maboresho yanayoendelea kufanyika katika hospitali hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyoielekeza serikali kuboresha huduma za matibabu ili kupunguza mzigo wa wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi.
Matibabu hayo ya upasuaji yanafanyika kwa gharama nafuu ambapo kwa wastani mgonjwa atalazimika kulipia gharama kati ya sh. 400,000 hadi 800,000.
Kwa upande wake Dk Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Januarius Hinju, amesema uchunguzi kwa kutumia matundu madogo ni rahisi tatizo la mgonjwa kubainika kwa haraka.
Amesema upasuaji huo unatumia muda mfupi kurejea kwenye hali ya kawaida kutoka wiki sita za upasuaji wa kawaida hadi wiki mbili za upasuaji wa matundu madogo na vigumu kwa mgonjwa kupata maambukizi.
Dk. Hinju amebainisha kuwa hadi juzi wagonjwa 20 wameshafanyiwa upasuaji na matibabu hayo yataendelea hata pale madaktari kutoka Marekani watakapoondoka nchini.