Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:42 pm

NEWS: HISA ZA NISSAN ZAPOROMOKA BAADA YA KUKAMATWA MWENYEKITI WAKE

Hisa za kampuni za kutengeneza magari nchini Japan Nissan na Mitsubishi, zimeshuka kwa haraka sana na hii ni baada kukamatwa kwa Mwenyekiti wa makampuni hayo Carlos Ghosn kwa madai ya matumizi mabya ya fedha.

Kukamatwa kwa Ghosn kumetikisa masoko ya biashara ya kampuni hizo ambazo zinatatengeza magari ya kuyauza duniani, hali ambayo pia imeathiri biashara katika masoko ya Tokyo.

Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hizo watakutana siku ya Alhamisi na kufikia uamuzi wa kumfuta kazi Bwana Ghosn ambaye sifa yake nzuri katika kampuni hiyo sasa, imepakwa tope kutokana na madai yanayomkabili.

Licha ya kukamatwa kwake, viongozi wa mashtaka nchini Japan hawajaeleza kwa kina kuhusu kukamatwa kwake, lakini ripoti zilizochapishwa kwenye Magazeti nchini humo zinaeleza kuwa, Ghosn alitumia vibaya zaidi ya Yen Bilioni tano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita