Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:40 am

NEWS: HATIMAYE UPELELEZI KESI YA BILIONEA MSUYA WAKAMILIKA

Dar es salaam: Hatimae upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika.

Akieieleza hayo leo Oktoba 22, 2018 mbele ya Mahakama Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Akitoa taarifa hizo, Wakili Mwita amedai kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika hivyo, wanaiomba Mahakama ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakia maelezo ya mashahidi na Vielelezo (Committal).

"Mheshimiwa Jalada la kesi hii limeshatoka kwa DPP na sasa tunalo hapa, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi na Novena amedai Mwita.

Kufuatia taarifa hiyo, wakili wa utetezi Peter Kibatala ameomba Mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe fupi ili wateja wake waweze kusomewa maelezo hayo.

Baada ya kusikiliza maelezo hayo Hakimu Simba amahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi mwaka huu.