Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:33 am

NEWS: HATIMAYE TAREHE YA UCHAGUZI NCHINI CONGO YATANGAZWA

Tume ya Uchaguzi nchini Congo (CENI), imetangaza kwamba uchaguzi wa urais utafanyika Desemba 2018, badala ya Aprili mwaka 2019.

Wakati huo huo upinzani umesema haukubaliani na tarehe hiyo mpya ya uchaguzi, huku ukimtaka Rais Josepha Kabila aondoke madarakani. Muhula wa Rais Kabila ulimalizika mwezi Desemba mwaka uliopita, na kuongezwa hadi Desemba mwaka 2017 baada ya makubaliano ya Saint- Sylvestre.

Kulingana na makubaliano ya Saint- Sylvestre yaliyoafikiwa mwaka jana, uchaguzi wa urais ulipangiwa kufanyika mwishomi mwa mwezi Desemba mwaka huu .

Wachanganuzi wa masuala ya siasa wanasema tume ya uchaguzi imechelewa kuandaa uchaguzi, hivyo kuwa na hofu ya kutokea vurugu nchini humo.

Tume ya Uchaguzi, CENI, imetangaza kwamba uchaguzi wa urais, wabunge na viongozi wa serikali za majimbo utafanyika tarehe 23 Desemba, 2018.

Tume ya Uchaguzi inasema matokeo ya muda yatatangazwa katika kipindi cha wiki moja baada ya kupiga kura (tarehe 30 Desemba), lakini matokeo kamili yatatangazwa tarehe 9 Januari, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila, mapema mwezi Novemba mwaka jana aliwahakikishia raia wake kwamba ataheshimu katiba ya nchi na kwamba hatawania urais katika Uchaguzi mkuu ujao.