- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HATIMAYE NDENGE YA AIRBUS A220-300 YAWASILI NCHINI
Ndege mpya Kubwa ya shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania imewasili leo jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais wa Tanzania John Magufuli Mchana wa leo.
Ndege hiyo,kimsingi imeundwa na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Airbus, ni ya muundo wa A220-300.
Ndege hiyo itakuwa na jina la Dodoma, mji mkuu rasmi wa Tanzania. Serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa kuhamishia shughuli zake zote jijini Dodoma.
Ndege hii urefu wake ni mita 38.7, na kwa jumla inaweza kuketi abiria 141.
Urefu wake kutoka chini kwenda juu ni mita 11.5, na upana wa mabawa yake ni mita 35.1.
Airbus 220-300 inaweza kusafiri umbali wa 5,920km safari moja, na inaweza kupaa ikiwa na uzani wa tani 67.6, na kutua ikiwa na uzani wa tani 58.7.
A220-300 ndiyo ndege kubwa miongoni mwa ndege za familia ya A220 na iliundwa kulenga soko la safai za ndege zinazowabeba abiria kati ya 130-160.
Ni ndege ambayo imeundwa kupunguza gharama ya matumizi yake ya mafuta kwa kila safari na pia kuwa yenye uwezo wa juu.
Injini zake zimepunguza matumizi ya mafuta kwa kila abiria kwa asilimia 20 ukilinganisha na ndege za awali za aina yake.
Ndege za A220 zimejengwa kwa vipande vinavyoweza kutengenezwa kwa haraka kiwandani iwapo vitahitajika wakati wa ukarabati.
Injini zake pia huwa za familia moja. Marubani waliozoea ndege aina ya A220-300 na A220-100 hawahitaji mafunzo zaidi kuweza kuziendesha.