- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HATIMAYE LISSU AANZA KUSIMAMA KWA MARA YA KWANZA
Nairobi: Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ameanza kupata nafuu na kurejea kwenye hali yake ya kawaida, hivi leo siku ya Boxing Day ameanza mazoezi yakusimama kwa mara ya kwanza kwa msaada wa madaktari.
Taarifa kutoka Hospitali ya Nairobi imeeleza kuwa Lissu kwa mara ya kwanza ameweza kusimama kwa msaada wa Physiotherapist tangu Septemba 7, mwaka huu alipopigwa risasi mjini Dodoma, hatua chache kabla ya kufika nyumbani kwake.
Akizungumza kutoka Hospitalini ya Jijini Nairobi Nchini kenya , Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS), amesema "Wapendwa wote wiki iliyopita niliwataarifu kwamba madaktari wangu wamesema nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania, "Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa mababa cheza kama inavyoonekana, hatua inayofuata nitawajulisheni," Aliongea Lissu
Lissu alipigwa Risasi tangu septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma nawatu wasio julikana ambapo alikimbizwa hospitali ya Mjini hapo saa chache kabla ya kupelekwa katika hospitali ya Nairobi Nchini Kenya ambapo anapatiwa matibabu mpaka sasa.