Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:26 pm

NEWS: HATIMAYE KENYATTA KUAPISHWA LEO BAADA YA HEKAHEKA ZA UCHAGUZI

Nairobi: Rais Uhuru kenyatta anatarajiwa kuapishwa leo siku ya juma nne (28.11.2017) baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39.

Takriban viongozi 13 barani afrika wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo inayompa mamlaka Kenyatta kwa awamu ya pili kuiongoza kenya.

Kwa upande wa Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi mwezi October ameitisha kufanyika kwa mkutano wa upinzani licha ya mkutano huyo kupigwa marufuku.

Uchaguzi wa mwezi Agosti ulifutiliwa mbali na mahakama kutokana na kile kilitajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.

salama umeimarishwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wakati wa siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa kwa awamu ya pili ya urais.