Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 8:50 am

NEWS: HATIMAYE KAVANAUGH AMEAPISHWA KUWA JAJI MKUU

U.S: Brett Kavanaugh aliapishwa kuwa jaji wa 114 wa Mahakama ya Juu ya Marekani, baada ya mjadala mkali sana kuhusu tabia chafu ya ngono na majibizano ya kisheria yaliyolitikisa baraza la Seneti na taifa zima.

Kuapishwa kwa jaji huyo mwenye umri wa miaka 53 kulikuja katika wakati ambapo Marekani imeingia kwenye kiwango cha juu kabisa cha mpasuko wa kisiasa kati ya waliompinga na waliomuunga mkono, huku ikihofiwa kuwa muhimili wa mahakama utaelemea zaidi kwenye siasa za mrengo mkali wa kulia kwa miongo kadhaa ijayo.

Jaji Kavanaugh aliapishwa kwenye sherehe ya kimyakimya na ya faragha muda mchache baada ya kupata ushindi mdogo kabisa kuwahi kushuhudiwa katika baraza la Seneti kwa takribani karne moja na nusu, huku waandamanaji wakipiga mayowe ya kumpinga nje ya jengo la mahakama.

Ushindi wa kura 50 dhidi ya 48 za kumpinga ulihitimisha mapambano ya muda mrefu ambayo taifa hilo tajiri lilijikuta likipambana nayo ndani yake, baada ya madai kuibuka kwamba aliwahi kuwashambulia kingono wanawake kadhaa miongo mitatu iliyopita - madai ambayo aliyakanusha vikali.

Tuhuma hizi ziliyabadilisha mapambano kutoka yale yanayotafautisha itikadi za kimahakama hado kuwa mashambulizi binafsi juu ya haki za wahanga na wateule na imani ya kutomtia mtu hatiani kabla ya uamuzi wa mahakama.