Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:37 am

NEWS: HATIMAE ZIMBABWE YAPATA RAIS MPYA

HARARE: Nchi ya Zimbabwe imeandika historia kwa kupata Rais mpya baada ya Rais Robert Mugabe kuhudumu kwa miaka 37 madarakani, Leo tarehe 24.11.2017 Emmerson Mnangagwa, ameapishwa kuwa rais mpya wa Zimbabwe mbele ya maelfu ya raia wa nchi hiyo. Mnangagwa, anakuwa rais wa pili wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika lililopata uhuru wake mwaka 1980.

Hatua hii imekuja mara baada ya kujiuzulu kwa rais wa zamani Robert Mugabe wiki hii baada ya kuongoza nchi hiyo kwa takribani miaka 37.

β€œ Mimi Emmerson Dambudzo Mnangagwa naapa kuwa rais wa Zimbabwe. Nitakuwa mwaminifu na kutii na kuilinda Katiba ya nchi,” alisema huku akishangiliwa.

Mnangagwa ameshangaliwa na maelfu ya raia wa nchi hiyo waliofika kushuhudia mabadiliko ya uongozini nchini humo.

Mbali na raia wa Zimbabwe, viongozi wengine wa Afrika wanashuhudia mabadiliko hayo akiwemo rais wa Zambia Edgar Lungu na Ian Khama wa Bostwana.

Rais wa zamani Zambia Keneth Kaunda na Rupia Banda nao pia wanahudhuria sherehe hizo jijini Harare.

Rais wa zamani Robert Mugabe hajaonekana katika sherehe hizo za kihistoria.

Wakuu wa jeshi sasa wanampigia saluti kamanda mpya wa jeshi na kusalimiana kwa mkono.

Ni Jeshi lililochukua jukumu kuu siku 10 zilizopita ambazo zilisababisha kujiuzulu kwa Robert Mugabe.

Bwana Mnangagwa amesema kuwa amekuwa akiwasiliana na makamanda wakati alipofurushwa na rais Mugabe kama naibu wake.

Alisema kuwa kulikuwa na mpango wa kutaka kumuua ndio sababu akaondoka nchini humo na kurudi siku ya Jumatano baada ya Mugabe kujiuzulu.