- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HATIMA YA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI KENYA NI LEO
Nairobi: Mahakama Kuu nchini Kenya Jumatano hii Oktoba 25 itasikiliza kesi ya dharura iliyowasilishwa na wapiga kura watatu wakiomba uchaguzi kuahirishwa.
kwa upande wa Kiongozi mkuu wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga amekuwa akiendeleza kampeni ya kuwashawishi wafuasi wake kutopiga kura.
Odinga anaituhumu Tume ya Uchaguzi kuwa imeshindwa kufanya mabadiliko muhimu yatakayowezesha Uchaguzi huo kuwa haki na Huru.
Odinga ameitisha maandamano ya nchi nzima kila siku kuanzia siku ya Jumanne huku akitarajiwa kutoa tangazo muhimu kwa wafuasi wake Jumatano hii Oktoba 25 siku moja kabla ya uchaguzi mpya wa urais.Upande wa Rais Uhuru Kenyatta amemaliza kampeni zake kwa kuomba kura huku akionya kuwa wale wanaopanga kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi huo watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati wiki iliyopita alisema Tume hiyo iko tayari kwa Uchaguzi huo lakini akasisitiza kuwa haamini iwapo utakuwa huru na haki.Siku ya Jumatatu, Chebukati alikutana na rais Kenyatta na kumhakikishia kuwa Uchaguzi huo utaendelea kama ulivyopangwa.
Katika hatua nyingine, Mabalozi wa mataifa ya nje nchini humo, wameshindwa kumshawishi Odinga kukubali kurejea katika Uchaguzi huo baada ya kukutana naye.Hali ya kisiasa nchini Kenya inaonesha wazi kuwa, kutakuwa na Uchaguzi maeneo kadhaa hasa yenye wafuasi wengi wa rais Kenyatta huku, ngome za Odinga hasa Magharibi mwa nchi hiyo zikisusia Uchaguzi huo.