Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:39 am

NEWS: HANSPOPPE KUPANDISHWA MAHAKAMANI LEO NA TAKUKURU

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Inakusudia kumfikisha Mahakamani leo Octoba 16 mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe baada ya Kumkamata Juzi mchana Uwanja wa Mdege akitokea Dubai.

Taasisis hiyo imemkamata jana Hanspoppe baada ya kumtangaza katika vyombo vya habari na kumtaka aripoti katika ofisi zake ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hanspoppe alikamatwa juzi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), saa 8.59 mchana akitokea Dubai.

Akizungumzia kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu, naibu mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema, “Ni kweli amekamatwa, alikamatiwa uwanja wa ndege mara tu alipowasili.”

Alisema walipata taarifa kwamba Hanspoppe anakuja nchini na wakawasiliana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji.

“Na vijana wetu wakawepo pale wanamsubiri na alipofika tu wakamkamata. Hanspoppe ataunganishwa moja kwa moja mahakamani.

Poppe kwa kushirikiana na Aveva na Kaburu walitoa maelezo ya uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo zilihusu klabu ya Simba kwamba imenunua nyasi bandia kutoka Kampuni ya Ninah Guangzhou Trading zenye thamani ya Dola 40,577 za Marekani, maelezo ambayo alidai kuwa yalikuwa ya uongo kwani nyasi hizo zilinunuliwa kwa Dola 109,499.

Kuhusu Lauwo, Mbungo alisema alifanya kazi ya ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Simba uliopo Bunju, Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa Sh249, 929,704 wakati akiwa hajasajiliwa katika Bodi ya Makandarasi Tanzania.