Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:35 am

NEWS: HANS POPPE ASEMA OKWI HADAI KITU CHOCHOTE SIMBA ALIPATA MALIPO YOOTE

Dar es salaam: Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa club ya Simba sc Hans Poppe amesema taarifa alizonazo ni kwamba, nyota huyo aliyesajiliwa msimu huu bado anaendelea na matibabu na si vinginevyo kama baadhi ya watu wanavyosema kuwa anadai pesa zake za usajili.

“Nilivyopata habari Okwi ni kwamba alikuwa bado anauguza shingo huko kwao sasa kama hayupo ni kwa sababu ya kuumwa” alisema Hans Poppe.

“Kama kuna maneno mengine zaidi ya hayo sidhani kama ni kweli kwa sababu ni mchezaji ambaye hadai kitu chocchote alipata malipo yake yote, wachezaji wote hakuna ambao wanadai kwamba afanye kwa makusudi kwa sababu hajalipwa haki zake.”

Kwa sasa Muda umepita bila Okwi kuonekana kwenye kikosi cha Simba, taarifa zinaeleza mchezaji huyo yupo Uganda akiendelea na matibabu baada kuumia shingo

Siku za karibuni iliripotiwa kwamba, Okwi ametia mgomo kwa sababu anadai pesa za usajili ambazo hajalipwa, hivyo kukaa kwake Uganda ni kushinikiza uongozi wa klabu hiyo umalizie kiasi anachodai.