- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALMASHAURI 12 MATATANI KWA FEDHA ZA MIKOPO TAMISEMI
DODOMA: Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo amezitaka Halmashauri 12 ifikapo Desemba 30 mwaka huu Kurejesha fedha walizokopa kwenye bodi ya mikopo ya serikali za mitaa.
Jafo ametoa agizo hilo leo mjini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema bodi ya mikopo ya Tamisemi imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.742 kwa halmashauri 54 lakini kuna baadhi ya halmashauri zimekuwa sugu kurejesha madeni hayo.
“Japo kuna halmashauri nyingi zimejitahidi katika kurejesha mikopo waliochukuwa lakini kuna halmashauri 9 zimeonyesha usugu uliopitiliza katika kurejesha mikopo hiyo ambazo ni zaidi ya sh bilioni 2 hazijarejeshwa kutoka katika halmashauri,”amesema Jafo.
Aidha amesema kuwa kati ya halmashauri 12 zilizokopa mikopo kwenye halmashauri ya Jiji la Mbeya na halmashauri ya mji Mbinga zimeonekana kuwa na deni kubwa kulinganisha na halamshauri zingine.
Amesema kuwa kitendo cha usugu katika urejeshaji wa mikopo kinazinyima fursa kwa halmashauri nyingine kupata mikopo.
“ Ninamuagiza mtendaji mkuu wa bodi ya mikopo kufanya ufuatiliaji ili wadaiwa wote waeweze kurejesha mikopo yao na wadaiwa sungu wawasilishe mikopo waliochukuwa kabla ya Desemba 30 ili taasisi iweze kutimiza majukumu yake,”amesema Jafo.
Amezitaka bodi ziangalie utaratibu wa kupitisha mikopo inayolenga ujenzi wa viwanda na uwekezaji katika Halmashauri ili kukuza ajira na uchumi wa viwanda.
Pia amezitaka bodi ziache kubweteka ijipange kimkakati wa kujenga uwezo mkubwa wa kutoa mikopo kwa halmashauri zilizomakini katika mapinduzi ya viwanda.