Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:52 am

NEWS: HALIMA MDEE AKAMATWA NA KUACHIWA NA JESHI LA POLISI

Dar es salaam: Mbunge wa Kawe, Halima James Mdee(CHADEMA), akamatwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na muda mchache kuachiliwa huru baada ya kuonekana amefanya mkutano bila kibali kutoka Jeshi Hilo maeneo ya Jimboni kwake (KAWE) jijini Dar es salaam.

Akizunguma na Jioni leo Agosti 1, 2018 , Mdee amesema alipigiwa simu na vijana wanaofanya biashara ya kutengeneza bustani wa eneo la Mzimuni, Kawe kwamba wamepewa notisi ya kuondoka. Amesema wakati anapigiwa simu, alikuwa Kunduchi katika ziara hivyo ikamlazimu kwenda kuwasikiliza wananchi wake.

Mdee alisema kuwa alipofika, alizungumza nao na kuwaeleza suala hili analishughulikia, kwani aliwasiliana na wizara ya ardhi, mipango miji na Tarura (wakala wa barabara za vijijini na mijini).”

Related image

“Ni kweli wale vijana wako eneo la barabara na wamenieleza hawana tatizo la kuondoka, lakini wanahitaji kuelekezwa wapi watakwenda kuendelea na shughuli zao.” amesema. Amesema baada ya kumaliza kuzungumza nao, aliondoka lakini alipofika mbele akaelezwa kuna watu wamekamatwa huko alipotoka. “Nikaona nirudi, nilipofika nikakuta baadhi ya wafanyabiashara na wanachama wanarushwa kichura chura, nikahoji kuna nini sikupata majibu yanayoeleweka.”amesema. Mdee amesema baada ya hapo, watuhumiwa hao waliokuwa chini ya ulinzi, wakapelekwa kituo cha polisi Kawe na yeye akatangulia kituoni.

“Nilipokuwa nakwenda, kama mita 20 nikaambia na mheshimiwa rudi, niliporudi nikaambiwa niko chini ya ulinzi, na kuniweka katika gari yao, tukaenda hadi kituoni na kuhojiwa kwa kufanya mkusanyiko usiokuwa na kibali,” amesema Mdee Hata hivyo, baada ya kuhojiwa wale wafanyabiashara na wanachama wa Chadema waliachiwa huru.