- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HAJI MANARA NA WENZAKE 18 WAACHILIWA KWA DHAMANA
Dar es Salaam. Msemaji mkuu wa Club ya Simba Sport club ya Jijini Dar es salaam Haji Manara na wenzake 18 kati ya 26 wameachiliwa kwa dhamana jana Usiku octoba 15, 2018.
Haji na wezake hao walikuwa wanashikiliwa na jeshi la polisi wakihusishwa na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji ‘Mo Dewji.
Haji Manara aliyekamatwa Oktoba 12, 2018 kutokana na kusambaza taarifa za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumwa na familia jambo ambalo si kweli.
Kauli ya kuachiwa kwa watu hao imetolewa leo Jumanne Oktoba 16, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.
Mambosasa amesema kufuatia kuachiwa kwa watu hao, polisi inaendelea kuwashikilia wengine saba. Hadi jana mchana watu 26 waliokuwa wakishikiliwa na polisi.
Familia ya Dewji Jana octoba15 ilitangaza dau la Sh1bilioni kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.
Dewji alitekwa na watu wasiojulikana Alhamisi Oktoba 11, 2018 saa 11:30 alfajiri wakati akiwa Hoteli ya Colosseum na hadi leo saa 3:45 asubuhi hakuna taarifa zozote za watekaji, lengo la kumteka wala fununu za alikohifadhiwa.