Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:28 pm

NEWS: FASTJET MBIONI KUFUNGIWA NA MAMLAKA YA ANGA TANZANIA

Mamlaka ya Mawasiliano ya Anga nchini Tanzania yamelipa siku 28 Shirika la ndege la Fastjet Airlines Limited maarufu kama Fastjet Tanzania kujieleza sababu zinazoweza kuzuia lisifungiwe kuendelea kutoa huduma hapa chini.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Safari za Anga Tanzania TCAA, shirika la ndege la Fastjet limekosa sifa ya leseni ya usafiri wa anga kwa sababu halina ndege zozote kwa sasa.

TCAA imesema ilitoa notice ya siku 28 ya kulitaka shirika hilo lisitishe mauzo ya tiketi kwa abiria. Na limeamuru shirika hilo kurejesha pesa kwa abiria hao au kuwatafutia usafiri mbadala katika mashirika mengine.

Mamlaka hiyo pia imeamuru waliopata hasara wafidiwe kwa mujibu wa sheria, na watoe mpango mkakati kwa nini wasifutiwe leseni ndani ya siku 28, pia ikitokea shirika hilo limefungwa basi walipe stahiki za wafanyakazi.

Fastjet tayari wametangaza kusitisha safari zake zote za mwezi Desemba na mwezi Januari. Na wameahidi kurejesha nauli za abiria wote kuanzia tarehe 20 mwezi desemba mwaka 2018.

Katika taarifa yao kwa umma Fastjet wameomba radhi kwa wateja wao bila kuweka wazi utaratibu wa awali kwa hifadhi za wateja hao mpaka watakapo rejeshewa nauli siku chache zijazo.

hirika la Fastjet lilianza kupata mushikeli wa kifedha baada ya mmiliki wa awali Fastjet PLC aliyekuwa na asilimia 49 kujiondoa ambapo shirika hilo liliuzwa kwa wawekezaji wa ndani.

Shirika hilo lilianzishwa mwaka 2011 likifahamika kama Fly540 Tanzania, lakini baada ya kununuliwa kikamilifu na Fly540 mwaka 2012, lilibadilishwa jina na kuwa Fastjet Tanzania.