- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: FACEBOOK YAOMBA RADHI TENA, KWA KUSHINDWA KUWALINDA WATUMIAJI WAKE
Mmiliki wa mtandao wa kijamii maarufu wa Facebook, Mark Zuckerberg, ameomba radhi tena akidai kuwa kampuni yake haijawajibika kwa kiasi kikubwa kudhibiti baadhi ya mambo kama vile habari za uzushi katika mtandao huo,kuingilia chaguzi na taarifa binafsi za wateja wake kudukuliwa.
Marck Zuckerberg akizungumza May 22 mbele ya bunge la Ulaya,ameelezea hatua ambazo Facebook imekuwa ikizichukua kuwa ni kuweka uhalali wa baadhi ya vitu ndani ya mtandao huo na kuhakikisha kuna mfumo unaolinda kudukuliwa kwa taarifa bionafsi za wateja.
''Kwa kabisa,kwa sasa unapotumia mtandao wetu,utaongozwa kwa na taarifa zako ili uweze kuingia na kupitia ukurasa wako na taarifa zake.
Jambo la pili ni kwamba kama utakuwa hujatumia mtandao wetu kwa muda wa miezi utatakiwa kuingia upya na kuonyuesha hatua za siri za usajili wako.Na tatu ni kwamba mwezi uliopita,tulionyesha program maalumu inayoonyesha wazi program nyingine na namna ya kuziruhusu ama kuzikatalia,jambo ambalo ni ulinzi kudukuliwa pia,
Na mwisho kabisa ni kwamba tunachunguza kila program ambayo tunaona kwa kiasi kikubwa inakiwango kikubwa cha taarifa binafsi za wateja wetu tangu 2014.Na pale tutakapoona kuna hali yoyote ya kutatanisha,tutawasiliana nao ama kuondoa kabisa program inayoingiliana na taarifa binafsi za wateja wetu na kuweka wazi kwa kila aliyeathirika kwamba program fulani inahusika''.Zuckerberg
Mjumbe kutoka Ubeligiji Guy Verhofstadt, amesema Zuckerberg anapaswa kufikiria na kulinda zaidi heshima yake.
''Lazima ujiulize mwenyewe kwamba unataka kukumbukwa kwa lipi,kama mmoja wa watu watatu muhimu katika masuala ya kimitandao,ambao ni Steve Jobs mwanzilishi wa appo na Bill Gates,mwanzilishi wa programu ya Microsoft na ambaye ameleta mabadiliko makubwa duniani na katika jamii yetu.Hilo ndilo jambo unalopaswa kujiuliza mwenyewe''. Guy Verhofstadt