Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:52 am

NEWS: ETHIOPIA YAPATA RAIS MWANAMKE KATIKA HISTORIA AFRIKA

Mwanadiplomasia Mzoefu Sahle-Work Zewde amechaguliwa na Bunge la nchini Ethiopia kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo.

Bi work amechaguliwa baada ya kujiuzulu ghafla kwa kiongozi aliyekuwepo madarakani Mulatu Teshome.

Bi Sahle-Work huyu ni mwanadiplomasia wamuda mrefu, sasa amekuwa kiongozi wa mkuu mwanamke barani Afrika.

Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo kunajiri wiki moja baada waziri mkuu Abiy Ahmed kuliteua baraza la mawaziri ambapo nyadhifa 10 kati 20 katika baraza hilo zimewaangukia wanawake

Katika hotuba yake ya kukubali wadhifa huo, rais Sahle-Work amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha amani, vyombo vya habari nchini vinaeleza.

Mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya waziri mkuu, Fitsum Arega, alituma ujumbe katika mtandao wa twitter kwamba uteuzi huo wa "kiongozi mkuu mwanamke haidhihirishi viwango vya miaka ijayo, lakini pia inafanya kuwa jambo la kawaida kwa wanawake kuwa waamuzi wakuu katika maisha ya umma".