- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ESTHER MATICO AWAKWAMISHA KINA MBOWE MAHAKAMANI
Dar es Salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kabisa kuwasomea maelezo ya awali viongozi wakuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kutokana na mshtakiwa wa tano, Esther Matiko kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo.
Lakini wakili wa mshtakiwa Peter kibatala alitoa udhuru wa mshtakiwa huyo leo Alhamisi Agosti 2, 2018, na kueieleza mahakama kuwa Matiko amepigiwa simu ya dharura kutoka katika shule anayosoma mwanaye mjini Nairobi, Kenya na kulazimika kwenda.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alimuhoji mdhamini wa mbunge huyo wa Tarime Mjini juu ya sababu za kwenda Nairobi na kujibiwa kuwa hata yeye hafahamu zaidi ya kuelezwa na Matiko kuwa anakwenda shule anayosoma mwanaye.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili wa Serikali mkuu, Faraja Nchimbi umemlaumu mdhamini huyo kwa kutojua sababu ya kilichompeleka mbunge huyo Nairobi, kutaka akirejea awe na uthibitisho.
"Upande wa mashtaka hatuna la kufanya ila kesi itakapotajwa inabidi aieleze mahakama pamoja na udhibitisho wa nini alichoitiwa huko" amesema Nchimbi.
Nchimbi aliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 6, 2018 huku Kibatala akiomba ipangiwe Agosti, 13, 2018 kwa kuwa Agosti 6 atakuwa na kesi Mahakama Kuu.
Hata hivyo, Mashauri alikubaliana na ombi la upande wa Jamhuri na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 6.
Hakimu Mashauri pia aliwaonya wanaompigia simu, bila kuwataja majina amesema akiwa kazini anakuwa hakimu na akiwa nyumbani anakuwa Mashauri.
“Nikiwa nyumbani ni Mashauri na nikiwa kazini ni Hakimu hivyo wanaonipigia simu nikiwa nyumbani huo sio utaratibu,” amesema hakimu Mashauri.
Mbali na Mbowe washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar); mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Wengine ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Musoma Vijijini, John Heche; mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Matiko.
Mbowe na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka 12 ikiwamo kuchochea ghasia, kukaidi amri ya polisi, uchochezi na uasi.
Wanadaiwa kufanya makosa hayo, Februari 16 wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana.
Katika tukio hilo, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini alipigwa risasi akiwa kwenye daladala, eneo la Kinondoni, Mkwajuni.