Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 9:26 am

NEWS: EBOLA YAENDELEA KUITESA DRC CONGO, WATU 27 WAPOTEZA MAISHA

KINSHASA: Vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa Ebola vimeongezeka mpaka kufikia 27, kwa mujibu wa chanzo cha hospitali Nchini Congo.

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na Ebola, inaendelea kuongezeka wakati chanjo dhidi ya ugonjwa huo ilianza kutolewa Jumatatu wiki hii.

Mmoja miongoni mwa wawili hao waliofariki kutokana na ugonjwa wa Ebola alikuwa katika mji wa Mbandaka (wenye wakazi milioni 1.2), ambao unatembelewa na wasafiri wengi wanaotumia njia ya bahari, nchi kavu na angani kuelekea au kutoka mji mkuu, Kinshasa.

Mwathirika mwingine, ambaye ni muuguzi, amefariki katika kijiji cha Bikoro, kaskazini magharibi mwa nchi, ambapo mlipuko wa Ebola uligunduliwa, Jessica Ilunga, msemaji wa wizara ya Afya ameliambia shirika la habari la Reuters.

Kesi saba mpya zimeripotiwa katika sekta ya Bikoro, Wizara hiyo imesema.

Mamlaka za afya ambazo zina matumaini ya kudhibiti kusabaa kwa ugonjwa huo, kwa ushirikiano na shirika la Afya Duniani walianzisha kampeni ya kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo hatari wa Ebola.