- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : DURU MPYA YA MAZUNGUMZO KUHUSU AMANI KUANZA NOVEMBA 27 NCHINI BURUNDI
Duru mpya ya mazungumzo ya amani ya Burundi kuanza Novemba 27
Duru mpya ya mazungumzo kuhusu mgogoro wa kisiasa wa Burundi inatazamiwa kuanza tena Novemba 27 hadi Disemba 8, mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Benjamin William Mkapa, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mgogoro wa kisiasa wa Burundi.
Duru za karibu na mpatanishi huyo wa mgogoro wa Burundi zinaeleza kuwa, duru ijayo ya mazungumzo ya amani ya Burundi itakuwa na maamuzi muhimu.
Mazungumo hayo yatakayodumu kwa siku 13 lengo lake ni kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao umepelekea raia wengi wa nchi hiyo kulazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani.
Hata hivyo hadi sasa bado haijaelezwa wazi ajenda hasa za duru ijayo ya mazungumzo hayo na hata pande zitakazoshirikishwa katika mazungumzo hayo. Serikali ya Burundi ilikataa kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja na upinzani ikiutuhumu kwamba, ulihusika katika jaribio la mapinduzi yaliyofeli ya mwezi Mei 2015.
Burundi ilitumbukia katika machafuko mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka 2015 baada ya chama tawala cha CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza, kugombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita kwa mara ya tatu mfululizo, machafuko ambayo yalishika kasi zaidi mjini Bujumbura. Wapinzani waliitaja hatua ya Rais Nkurunziza kushiriki katika uchaguzi huo kwamba ilikiuka katiba na hati ya makubaliano ya amani ya Arusha Tanzania lakini serikali ya Bujumbura imesema haijakiuka sheria.