Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:35 am

NEWS: DR. SLAA AULA ATEULIWA KUWA BALOZI (IFAHAMU HISTORIA YAKE)

Dar es salaam: Alikuwa katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Dr. Wilbrod Peter Slaa ameteuliwa kuwa balozi na Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dr. John Pombe Maguli.

Dr. Slaa alikuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chama kinachoongoza mpaka sasa kambi rasmi ya upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alijiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu na uanachama wa Chadema mwaka 2015 baada ya ujio wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye alipewa nafasi ya kugombea urais mwaka huo.

Alikuwa mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili kwa asilimia 27.05 ya kura zote, akiachwa na Jakaya Kikwete wa CCM aliyeongoza kwa kupata asilimia 62.83, kadiri ya matokeo rasmi ambayo hayajasadikiwa na wananchi wote.

Kabla ya kugombea urais mwaka 2010 alikuwa mbunge wa Karatu miaka 1995-2010; baada ya kugombea Urais akawa si mbunge tena.

Slaa alianza kuwa kiongozi tangu alipokuwa mwanafunzi pale Kipalapala ambapo alichaguliwa kuwa rais wa wanafunzi; mapadri wanasema alikuwa mmoja wa viongozi wazuri sana kupata kuongoza Kipalapala.

Pia Slaa amewahi kua msaidizi wa askofu na mkurugenzi wa maendeleo katika Jimbo Katoliki la Mbulu.

Slaa alijitoa kwenye upadri mwaka 1991. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maaskofu kadhaa, Slaa alifanya hivo kwa kufuata taratibu za Kanisa Katoliki na aliacha mwenyewe bila kufukuzwa, kushinikizwa ama kupewa onyo.

Aliingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge mwaka 1995 akiomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi kupitia tiketi ya CCM na alishinda katika kura za maoni za chama hicho. Vikao vya CCM vilipokutana Dodoma vikamuengua na kumweka tena mbunge anayemaliza muda wake, Patrick Qorro. Wananchi wa Karatu wakamuomba agombee ubunge kupitia chama kingine na ndipo Slaa alipambana na wagombea wa vyama vingine kama CCM, CUF, NCCR MAGEUZI, UDP na aliwashinda wote kwa kupata asilimia 52, akifuatiwa na mgombea wa CCM aliyepata asilimia 44.