- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DR. MASHINJI AMJIBU RAIS MAGUFULI JUU YA UTOAJI TAKWIMU
Dar es salaam: Katibu mkuu wa chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA Dr Vincent Mashinji amehoji juu ya udhibiti wa utoaji takwimu nchini Tanzania na kusema kuwa ipo haji kama serekali kujitathimini upya badala ya kufukuza wafanyakazi wake ili hali wanao toa Data wanajua sehemu sahihi pa kuzipa takwimu hizo.
"Kudhibiti Takwimu kunalenga nini hasa? Sababu katika tafiti tuna published na unpublished data. Tafsiri yake ipo wazi tu. Nadhani ni vyema kama Taifa tujitafakari UPYA kwani watumia data wanajua wapi pa kuzipata na hakuna haja ya Serikali kutokwa povu ikifukuzana na watu wake". alisema Mashinji
Desemba 20, 2017 wakati wa ufunguzi wa Jengo la Takwimu Mjini Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli alitoa onyo juu ya watu wanao toa taarifa za uwongo kuchukuliwa hatua mara moja na kuwaomba watanzania kujifunza kuheshimu takwimu zinazotolewa na Shirika la takwimu la Tanzania National Bureau of statistics
"Natoa onyo kwa wale wanaotoa takwimu za uongo hivyo naagiza mamlaka husika wachukue hatua dhidi ya watu wa namna hiyo”
"Hata mtu akija na takwimu za kupikwa kwamba vyuma vimekaza, mpelekeni Mahakamani akaeleze ametoa wapi hizo takwimu. Ninaomba kurudia tena, Watanzania tujifunze kuheshimu takwimu. Ukitoa takwimu za uongo athari yake ni mbaya sana kwa Taifa" alisema Rais Magufuli