Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:40 am

NEWS: DR. CHENI ASIMULIA JINSI LULU AVYOPOKEA HUKUMU YAKE

Dar es salaam: Muigizaji wa muda mrefu nchini Tanzania Mukhsin Awadh maarufu kama Dk Cheni amesema kuwa Lulu alijua kuna kitu chochote kinaweza kutokea kwenye hukumu yake kabla ya kusomwa “Kusema ukweli Lulu alijua lolote linaweza kutokea ila la kufungwa ni kama hakulipa kipaumbele sana, jaji alipomaliza kusoma hukumu alishtuka kama sisi wengine wote lakini ajabu alikuwa wa kwanza kurudi katika hali ya kawaida na kutoa kauli za ujasiri,” anasema Dk Cheni

kwa mujibu wa Dr Cheni amesema Lulu alisema yeye kama yeye hawezi kupingana na maamuzi ya mahakama kwani anahisi kuwa hukumu ile ilikuwa mipango ya mungu: "Sipingani na maamuzi ya Mungu, haya ni maamuzi yake na nimekubaliana nayo. Ana makusudi yake kunipa hiki kilichotokea leo".
Anasema kingine alichowaambia ni kuachana na masuala ya kukata rufaa kwa sababu bado hatakuwa huru: "Acheni miaka miwili siyo mingi, sitaki kupingana na mahakama , naheshimu maamuzi ya mahakama, acheni nitumikie kifungo changu. "


Dk Cheni ambaye amekuwa karibu na mwigizaji huyo katika kipindi chote tangu mwanzo wa kesi hiyo mara baada ya kifo cha kanumba mpaka hapo lulu aliposomewa hukumu yake
Mapema wiki hii mwigizaji huyo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, Aprili 7,2012.