Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:45 pm

NEWS: DKT. NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA.

JIJINI DOM: Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kuhakikisha mashine ya kutolea huduma za X-ray inafanya kazi ndani ya siku 14.

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kuangalia na kujiridhisha na hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali hiyo leo jijini Dodoma.

"Ifikapo Septemba 21 nataka kuona mashine ya kutolea huduma za X-ray na vifaa vingne viwe tayari kutoa huduma kwa wananchi wa Dodoma na maeneo yanayoizunguka kwani Hospitali hii ni tegemezi kwa wakazi wa mkoa huu la sivyo hatua stahiki zitachukuliwa bila ya kumuonea mtu haya" alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha,Dkt. Ndugulile ametoa siku 30 kwa uongozi wa hospitali hiyo kukarabati jengo la bima ya afya baada ya kukagua na kutoridhishwa na muonekano wake kwani linaleta kero kwa wateja wanaokwenda kupata huduma Hospitalini hapo.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameonekana kukerwa na uzembe wa watendaji wa Hospitali hiyo na kusababisha kuwakemea vikali na kuhaidi maagizo aliyoyatoa yasipotekelezwa kwa wakati hatua za kinidhamu zitakuchululiwa kwa vitendo.

Wakati huo huo dkt.Ndugulile ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuwarudishia fedha wagonjwa walizotumia kununua dawa pamoja na sindano kwenye maduka yaliopo nje ya hospitali hiyo ilihali wana vifaa hivyo takribani ya kutosha miezi sita kwenye stoo yao