- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : DKT HARRISON MWAKYEMBE ATOA SALAMU ZA POLE KWA UONGOZI WA CLOUDS MEDIA GROUP
Waziri wa Habari sanaa utamaduni na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametuma salamu za pole kwa viongozi na wafanyakazi wa Clouds Media group kufuatia ajali ya sehemu ya jengo la kituo hicho kuungua kwa moto
Jengo lilo la Clouds media liliungua juzi mchana katika baadhi ya sehemu za kurushia matangazo,ambapo mpaka sasa imeelezwa chanzo cha moto huo hakijajulikana
Waziri mwenye dhamana ya habari Dkt Mwakyembe ametuma salamu za pole kwa uongozi mzima wa kitua hicho cha habari kwa tafrani nzima iliyowakumba,ambapo pia waziri mwekyembe ameoneshwa kushtushwa na taarifa hizo za kuungua moto kwa jengo hilo
Taarifa za kuungua kwa jengo hilo amezipokea akiwa mkoani Iringa ambako ameenda kwa ajili ya ziara fupi ya kikazi,huku akizitaka taasisi husika za uchunguzi kuanza kazi ya ya uchunguzi mara moja ili kubaini chanza cha moto huo
Aidha Dkt Harrison Mwakyembe amesema amelishukuru jeshi la zimamoto kwa kuwahi eneo la tukio na kuweza kudhitibiti sehemu ya moto huo,ili usiendelee kuleta madhara
kwa upande wake,Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi Clouds media,ndugu Ruge Mutahaba,pamoja na kukubwa na janga hilo ameahidi,matangazo ya Radio na Television yataendelea kuwa hewani kama kawaida
Ndugu Ruge,amesema lengo lao ni kuhakikisha wanatenda haki na kulinda usawa kwa wasikilizaji na watazamaji wa kituo hicho cha habari.