November 28, 2024, 4:36 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DKT FEKI ANASWA DAR.
DAR ES SALAAM: Wakili feki aliyetambulika kwa majina ya Bw. Jeremiah Ragita amekamatwa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.
Pichani hapo juu ni Bw. Jeremiah Ragita aliyejifanya kuwa Wakili akitokea Kampuni ya Sheria ya Faithful Attorney Advocates kwa mujibu wa Naibu Msajili, Mahakama ya Ardhi, Mhe. Frank Mahimbali anasema Wakili huyo feki alikamatwa mapema Novemba 08 katika Mahakama hiyo akimsimamia Mleta maombi Nunu Mhusin Mkwata.
Mhe. Mahimbali anasema kuwa upande wa pili ambao unasimamiwa na Wakili Maros Gabriel kutoka Kampuni ya Sheria ya 'Common Law Chambers' ulimtilia shaka Bw. Jeremiah Ragita kama kweli ni Wakili ndipo alipofanya upekuzi kwenye Ofisi ya TLS na kuambiwa kuwa hawana jina hilo.
Hata hivyo Mhe. Mahimbali alienda mbali na kumuandikia barua Msajili wa Mahakama Kuu (RHC) na kujibiwa kuwa hakuna Wakili aliyesajiliwa kwa jina hilo.
Kwa mujibu wa Naibu Msajili kesi hiyo ilipoitwa mbele ya Mhe. Jaji Crencesia Makuru, Wakili Maros alimueleza Mhe. Jaji kuwa mwenzake wa upande wa pili sio Wakili na kisha akatoa vielelezo kutoka katika Ofisi ya Msajili Mahakama Kuu na Ofisi ya TLS ndipo Bw. Ragita akakiri kuwa yeye si Wakili.
Hata hivyo Bw. Ragita alikamatwa na kupelekwa Polisi Kituo cha Kati (Central Police) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hatua stahiki za kisheria.
Mahakama inapinga vikali vitendo vya ulaghai (Mawakili feki, vishoka) vinavyofanywa na baadhi ya Wananchi kwa lengo la kujipatia kipato.
Huyo wakili alibainika si baada ya kumsalimia Jaji 'shikamoo' kama inavyosemwa katika vyanzo vingi vya taarifa/habari bali alianza kushtukiwa muda mrefu kwa vitendo visivyo vya ki-wakili alivyokuwa akimfanyia wakili Gabriel.
Alikuwa akishindwa hoja mahakamani anamkunja shati Gabriel wakitoka mahakamani mbele za wateja huku akimtisha waziwazi.
Upande wa pili ukaamua kuandika barua kwa Msajili kuomba status yake ndipo msajili akajibu kwamba sio wakili.
Baadae ndipo Gabriel akamweleza jaji kwamba anamtilia shaka kwamba sio wakili na ana barua ya Msajili inathibitisha hilo, akaionesha. Jaji akaanza kumhoji jamaa, majibu yaliyomshtua jaji ni pamoja na kusema kwamba “Roll number” yake ni Elfu Ishirini na kitu wakati “Roll number” hazijafika elfu 10.
Wakili huyo feki pia alidai kaapishwa mwaka 2004 wakati miaka hiyo ndio kwanza “Roll Number” zilikuwa chini kabisa.
Kwa ufupi, hivyo ndivyo alivyobainika.
#Jamiiforums.