Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:41 pm

NEWS: DK KIGWANGWALA AFUTA VIBALI VYA UWINDAJI WA MAKAMPUNI.

DODOMA: Siku chache mara baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri,Waziri wa maliasili na utalii Dkt Khamis Kigwangwala ametoa agizo la kufutwa kwa vibali vyote vya uwindaji wa makampuni ili kupisha utaratibu mpya wa ugawaji wa vitalu kwa njia ya mnada.

Sekta ya maliasili na utalii ni miongoni mwa sekta zinazoliingizia taifa mapato makubwa ambapo sekta hiyo imekuwa ikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukidhiri kwa vitendo vya ujangili wa wanyamapori pamoja na changamoto ya wananchi kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi

Akizungumza na wadau wa sekta ya maliasili na utalii,Waziri Dkt Khamis Kigwangwala amewataka watendaji wa wizara hiyo wakamilishe masharti mapya ya uwindaji wa wenyeji huku akifuta vibali vya uwindaji wa makampuni mpaka utaratibu mpya utakapokamilika

Kuhusu swala la udhibiti wa vitendo vya ujangili waziri Dkt Kigwangwala amesema serikali imeimarisha kitengo cha kukamata majangili ndani na nje ya nchi na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa majangili


Baadhi ya wadau wa sekta ya maliasili na utalii akiwemo mkuu wa wilaya ya Chemba Simon Odunga wamesema kuwa kukidhiri kwa vitendo vya uvamizi katika hifadhi ni moja ya changamoto inayoikabili sekta hiyo


Baadhi ya wananchi mkoani wakatoa maoni yao juu ya sekta ya maliasili na utalii huku wakikiri kuwa moja ya changamoto inayoikabili sekta ni uvamizi holela unaofanywa na wananchi katika maeno ya hifadhi


Licha ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi barani Afrika yenye vivutio vingi vya utalii na maliasili bado wito unatolewa na wadau kuhakikisha vivutio hivyo vinatangazwa na kulindwa kwa maslahi ya Taifa