- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DIAMOND AMPA SHAVU NONO ALIKIBA
Dar es Salaam: Msanii Nyota wa muziki kutoka Afrika mashariki Naseeb Abdul maarifu kama DiamondPlatnumz ametangaza kuanza rasmi kwa tamasha la Wasafi Festival ambalo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 24, mwaka huu mpaka Desemba mwisho itafanyika ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo November 5, 2018 Diamond amesema kuwa tamasha hilo litahusisha wasanii Kibao, Huku akiongezea kwa kusema kuwa wasanii wale wote wanaofanya vizuri hapa nchini watakuwepo huku akisema anatamani hata Ali Kiba naye awepo katika tamasha hilo
"Natamani kaka yangu Ali Kiba naye awepo na ninaamini uongozi wangu utaanza mazungumzo naye na huko alipo kama anafuatilia wasafi ajue tungehitaji uwepo wake, kwani inabidi tutoke kwenye muziki wa mabifu na tuingie katika kutengeneza hela na kuisaidia jamii inayotuzunguka," amesema.
Diamond amesema kwa kuanzia tamasha hilo lenye kauli mbiu ya 'Mchezo usiuchezee wewe Kabisa' litafanyika mkoani Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Diamond alitaja mikoa mingine itakayofuata kuwa ni Iringa ambapo litafanyika Novemba 30 na kufuatiwa na Morogoro na mikoa mingine itatangazwa hapo baadaye huku Nairobi likitarajiwa kufanyika Desemba 31 mwaka huu .
Amesema tamasha hilo mbali na kujumuisha wasanii wa ndani pia wataletwa wasanii wa nje ikiwemo kutoka nchini Nigeria na Marekani ambao wamekuwa wakifanya nao kazi kwa karibu.
Diamond, mkali wa vibao vya Mbagala, Sikomi, Baila na African Beauty amesema fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo nyingine zitasaidia jamii ya mkoa husika ikiwemo kununua sare za wanafunzi katika shule na kutoa mitaji kwa wakina mama 200.
"Tunataka tamasha hili kila linapofika liwanufaishe wakazi wa pale si kwenda tu kuchukua hela zao na kusepa, na kwa kuanzia tutawasaidia kina mama," amesema.