Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:28 am

NEWS: DIAMOND ADHIBITISHA KUMLIPIA HAWA MILIONI 50 ZA MATIBABU

Msanii Nyota wa Muziki Africa Mashariki Diamond Platnumz hatimaye amesikia kilio cha wengi baada ya Jana Sept. 28 kudhibitisha kuwa yupo kwenye hatua za mwisho kugharamia Matibabu ya Mwanamuziki mwenzake Hawa.

Kupitia Ukurasa wake wa twitter Diamond alisema kuwa hakupenda kuiweka inshu hii njee(Public) au kutangaza kwa sababu watu wangehisi anatafuta kiki na wakati alitaka kujitolea kama msaada.

Mwanamuziki huyo mkali wa single Kibao ikiwemo Iyena aliyomshirikisha Rayvanny amesema kuwa matibabu ya mwanamuzi huyo si chini ya Milioni 50 lakini ameahidi kukabiliana na gharama hiyo.


Hawa na Diamond wamewahi kuwa marafiki katika safari ya kimuziki mpaka miaka ya 2010 walipotoa hits song ya nitarejea iliyomfanya Diamond kuongeza idadi kubwa ya mashabiki(fanbase) katika muziki wake.

Hawa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Inni na amekuwa akiomba msaada wa fedha akihitajikia kwenda Nchini India kwa matibabu zaidi.

Mama yake na hawa alinukuliwa akisema kuwa ugonjwa wa mwanae ni mkubwa sana kwa sababu Kila mara tumbo la mwanae linajaa maji mpaka linamfanya mwanamuziki huyo kuonekana kama anaujauzito wa miezi tisa.


Imeandikwa na Deyssa h. Issa

Na Kuhaririwa na Japhet kyoko

Muakilishi Publisher