Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:48 pm

NEWS: DHAMANI YA WABUNGE WA CHADEMA YAGONGA MWAMBA

Morogoro. Leo asubuhi Tarehe (05.12.2017) Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imeshindwa kuwapa dhamana wabunge wawili wa CHADEMA Susan Kiwanga na Peter Lijualikali pamoja na washtakiwa wengine 36 baada ya kuibuka kwa hoja za kisheria Upande wa mashtaka na ule wa utetezi unavutana kuhusu hati ya kiapo ya kupinga dhamana iliyowasilishwa mahakamani hapo.

Kutokana na mvutano wa kisheria, hakimu Ivan Msack ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano Desemba 6,2017 ili kutoa fursa kwa pande zote mbili kujibu hoja kuhusu hati hiyo kwahiyo washtakiwa hao wamerejeshwa rumande mpaka hapo kesho.


Wabunge hao wanakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Kata ya Sofi iliyopo wilayani Malinyi.
Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala, Ignas Punge, Fredrick Kiwelo na Bartholomew Tarimo.
Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Edga Bantulaki na Sunday Hyera.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Frederick Sumaye, wamehudhuria katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ambako uamuzi wa dhamana ya wanachama wa chama hicho utatolewa.

Wengine waliofika mahakamani ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na wa Viti Maalumu, Devota Minja.