- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC SHEKIMWERI AZINDUA ZOEZI LA UOGESHAJI MIFUGO.
MPWAPWA DODOMA: Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri amezindua zoezi la Uogeshaji Mifugo huku akizitaka kamati za majosho kwa kushirikiana na serikali za vijiji kusimamia sheria zilizopo kikamilifu ikiwemo kila mfugaji kuhakikisha anaogesha mifugo yake.
Shekimweri ametoa agizo hilo leo wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo lililofanyika Kijiji cha Kisokwe mkoani Dodoma.
“Naomba nitumie fursa hii kuwasisitiza umuhimu wa kuwa na mifugo yenye afya bora,kamati za majosho kwa kushirikiana na serikali za vijiji tunzeni takwimu na wapigeni faini wale wasiopeleka mifugo yao,”alisisitiza Shekimweri.
Amesema serikali imepeleka kiasi cha lita 137.5 ya Dawa ya Paranex kwa ajili ya kuogesha mifugo.
“Dawa hii itaogesha mifugo kwenye majosho 22 yaliyopo hapa Mpwapwa ambapo kila josho litapatiwa lita 6.25 kwa ajili ya kuogesha mifugo ili kuongeza tija,”alisema Shekimweri.
Shekimweri ametumia nafasi hiyo kuwatakia heri katika sikukuu ya Christmas na mwaka mpya wakazi wa Mpwapwa na kuwahimiza kuzingatia kilimo cha kisasa ikiwemo kupanda mazao yatakayoimarisha lishe kwa mama wajawazito na watoto wenye umri usiozidi miaka miwili.