Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:33 pm

NEWS: DC MUKUNDA ''HATUWEZI KUENDELEA KUWAVUMILIA WALE WOTE WANAOHARIBU MISITU YETU''.

ZENJELI DODOMA: Mkuu wa wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Mwanahamisi Mukunda amesema Wilaya yake haitamvumilia mtu yoyote anakayehusika na uharibifu wa mazingira, endapo atabainika hatua kali zitachukuliwa zidi yake.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya askari wa jeshi la akiba (Mgambo) yaliyofanyika katika Kijiji cha Zejele kata ya Nondwa wilaya ya bahi Mkoani Dodoma Mkuu huyo amesema hadi sasa ni wiki la pili la mwezi Desemba mvua hazijanyesha Katika Mkoa huo hii ni kutokana na watu kuharibu mazingira hali inayopelekea mvua kunyesha kwa shida na kusababisha ukame.

‘’Lakini kingine kata hizi mbili ikiwemo Nondwa bado kunauharibifu mkubwa wa mazingira unaendeleabado miti mingi inakatwa Hususani Chikopelo sasa wananchi wameanza kuingia hata kwenye maeneo ya hifadhi wanakata mkaa, wanakata mbao na zinatoroshwa usiku hii kupelekea hadi saivi Dodoma hakuna dalili ya Kupata Mvua,’’Amesema Mkuu Huyo.

Mbali na hayo Mkunda amewatahadhalisha wananchi wa kijiji hicho kuhakikisha kila nyumba inajenga choo kabla ya tarehe 11 mwezi huu na kudai kuwa lengo kuu kujiepusha na magonjwa kama kipindupinduzi pindi Mvua zitakaponyesha.

Pia amesema kama watu hawatakuwa na choo inapelekea kuhatarisha afya yako na kudai kuwa maendeleo hayawezi kuja kama watu watakuwa na afya mbovu.

Akizungumzia mafunzo hayo amesema yamekuwakuwa na faida nyingi sana hasa katika kudumisha uzalendo wa taifa nakuwataka vijana wahiohitimu kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo lililokusudi na si kinyume na kusudio la mafunzo hayo na kuongeza kuwa watawashughulikia vijana 11 ambao walijitoa katika jeshi hilo kabla mafunzo kuisha.

Awali Mkurungezi wa wilaya hiyo Leo Mavika amewahasa vijana hao kutumia mafunzo hayo kuwafundisha vijana wengi ili kukuza utaifa na uzalendo wa Taifa lao na kuongeza kwa kusema vijana wengi wa sasa wameanza kupoteza uzalendo wao.

‘’Tanzania yetu ni nzuri sana lakini zaidi zaidi sana Tanzania ya sasa chini ya uongozi wa Rais Dk John Pombe Magufuli ni nzuri na inaenda kuwa nzuri zaidi kwa maana hiyotumuunge Mkono katika kulinda rasimali zetu zisiporwe na kunyang’anywa na Warafi ili tuweze kuzitumia sisi wenyewe kwa manufaa ya Taifa letu’’, amesema Mkurungezi huyo.

Mafunzo ya Askari wa jeshi la akiba Kijiji cha Zejele kata ya Nondwa wilaya ya Bahi yamefanyika kwa muda wa miezi mitano takbani vijana 78 amehitimu Mafunzo hayo .