- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC MTATURU KIJIJI KWA KIJIJI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI NA KUZITATUA.
IKUNGI SINGIDA: MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida mh Miraji Mtaturu ameendelea na ziara yake katika vijiji vya Utaho,Kituntu na Musambu.
Ziara hiyo pamoja na mambo mengine ina lengo la kuhamasisha Maendeleo, Kilimo sambamba na kusilikiliza kero za wananchi na kuzitatua .
Akiwa katika shule ya Sekondari ya Miandi amekutana na Bodi ya Shule,walimu na viongozi wa Kata wakiongozwa na Diwani na kuonyesha kutoridhishwa na muenendo wa bodi hiyo baada ya kubaini kuwa hawajakaa vikao tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2009.
Kufuatia hali hiyo amemuagiza Mkuu wa Shule Mwalimu William Ipini kumpatia maelezo kabla ya tarehe 26 octoba mwaka huu saa 5 asubuhi.
"Hii bodi inapaswa kutimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kukaa vikao vyake mara 4 kwa Mwaka,Kaimu Mkurugenzi nakukabidhi faili hili likague na unipe taarifa kama bodi inafanya kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya Elimu,"aliagiza Mtaturu.
Ili kuongeza ari na kujituma zaidi mh Mtaturu amewakabidhi walimu wawili wa kujitolea sh. 100,000 kama motisha na sh 100,000 kwa walimu wa Sekondari ya Miandi kwa ajili ya chai wanapokuwa kazini.
Pia amemwelekeza mkurugenzi kutengeneza madawati 20 na kuweka mpango wa kuwajengea nyumba 1 ya walimu.
Akiwa katika kijiji cha Utaho amewapongeza wananchi kwa kutimiza wajibu wao wa kujenga shule mpya ya Msingi itakayoitwa Samamba kwa kushirikiana na Mh Elibariki Kingu(mb)Singida Magharibi,Diwani Kata ya Kituntu na Serikali ya Kijiji na hivyo kumuelekeza mkurugenzi kupitia idara ya elimu kusimamia usajili wa shule hiyo.
"Hongereni sana hapa naona mmeshakamilisha madarasa manne, mawili yapo katika hatua ya upauaji, nyumba moja ya mwalimu na matundu ya vyoo 14 mmeshakamilisha pia, mkurugenzi endelea na ukamilishaji wa madarasa mawili na madawati 20 ili kukamilisha mahitaji ya hapa,"alisema Mtaturu.
Akizungumzia migogoro ya ardhi amewataka wananchi kumaliza migogoro hiyo na kuahidi kuwashughulikia madalali wa ardhi ambao wamekuwa chanzo cha migogoro na uvunjifu wa Amani.
Katika sekta ya afya amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Musambu kwa kutenga eneo la kujenga zahanati na kutengeneza matofali elfu 2,690 na hivyo kumwelekeza mhandisi wa ujenzi kwa kushirikiana na idara ya ardhi kupeleka ramani waanze kuchimba msingi ili ujenzi uanze mara moja.
Ametumia ziara hiyo kuwasisitiza wananchi kuzingatia kalenda ya msimu wa kilimo na Watendaji,maafisa Ugani,Viongozi wa Vijiji na Vitongoji wasimamie kila mwananchi atimize wajibu wake ikiwa ni pamoja na kukagua mashamba ili lengo la wilaya la kuzalisha chakula cha kutosha lifikiwe.
Katika ziara hiyo Wananchi wa vijiji vya Utaho,Kituntu na Musambu wamemshukuru Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapelekea umeme wa REA na sasa wameanza kuutumia ambapo mh Mtaturu amewasisitiza wananchi kulipia sh elfu 27,000 ili waitumie fursa hiyo kuunganishiwa umeme majumbani mwao.
Ziara hiyo inaendelea katika vijiji vingine ikiwa imebeba dhana ya serikali ya kuwafikia wananchi na kubaini changamoto zao na kuzitatua.
"IkungiYetuSote#