- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC MTATURU AWASAIDIA WANANCHI WAKE KUPATA MITAJI.
DAR: Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu amefanya mazungumzo na Baraza la Wawezashaji Kiuchumi ili kuona namna ya kuwasaidia wananchi kupata mitaji ya kuendeshea shughuli za kiuchumi.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar-es-salaam Mtaturu amekabidhi maandiko matatu ya vikundi vya wakulima,wachimbaji wadogo wa madini na wafugaji wa Nyuki.
Akikabidhi maandiko hayo amesema dhamira ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dokta John Magufuli ni kuwawezesha wananchi wabadilishe kilimo cha mazoea wanachotumia ili wapate mbegu bora.
"Dhamira ya serikali yetu kuwatafutia wakulima wetu masoko ya uhakika ikiwemo kuongeza thamani ya mazao yao,wachimbaji wadogo wa madini nao tuwawezeshe kuchimba kisasa ili wapate faida ya maliasili zetu na wakulima wasitegemee kilimo cha mvua tu, hii ndio dhamira ya mheshimiwa Rais wetu Dokta John Magufuli,"alisisitiza Mtaturu.
Kwa upande wao mwenyekiti wa baraza hilo dokta John Jingu na mtendaji mkuu Hajat Ben'g Issa wamempongeza mkuu huyo wa wilaya na ujumbe wake kwa kuamua kuwapigania wananchi wake.
"Sisi tunawaahidi kuwaunganisha kwenye taasisi na mifuko inayohusika na uwezeshaji ili kuwasaidia wananchi kubadili aina ya shughuli zao kiuchumi ziwe bora zaidi na zenye tija,"walisema viongozi hao.