- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC MTATURU ASHIRIKI UJENZI WA MADARASA.
IKUNGI SINGIDA: Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu ameshiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi ya Mankumbi iliyopo kata ya Kikio wilayani humo huku akitoa mwezi mmoja wa kukamilisha madarasa manne ili kuondoa upungufu uliopo.
Hatua hiyo inafuatia baada ya ziara yake aliyoifanya katika shule hiyo mei 15 mwaka huu na kukuta madarasa yakiwa katika hali mbaya.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa wilaya Mtaturu aliagiza Halmashauri kutoa pesa haraka kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na kuhamasisha wananchi kuchangia nguvu kazi ikiwa ni pamoja na kusogeza mchanga na mawe.
Akizungumza shuleni hapo amesema tayari halmashauri wameshachangia shilingi milioni 10 na kuahidi kuongezea shilingi milioni 10 nyingine ili isaidie vifaa vya viwandani kukamilisha madarasa manne yaliyoanza kujengwa.
"Naiagiza kamati ya shule na serikali ya kijiji kwa pamoja msimamie ujenzi huu sasa ili tuondoe changamoto iliyopo ya ukosefu wa madarasa ya kutosheleza idadi ya wanafunzi wapatao 369 tulionao shuleni hapa,"alisema Mtaturu.
Amewaahidi kupeleka wafadhili watakaojenga madarasa manne na nyumba tatu za walimu na kuwapongeza wananchi kwa moya wao wa kujitolea kwenye kujiletea maendeleo kwa kuwa hayo ndio mambo yanayotakiwa.
Akisoma taarifa ya shule mwalimu Abdallah Mwinjuma amesema matokeo ya shule kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ni mazuri na kueleza changamoto walizonazo kuwa ni pamoja na upungufu wa walimu na miundombinu ya shule.
"Nakushukuru mheshimiwa mkuu wa wilaya kwa kuwa tayari kutatua changamoto zetu haraka, niwaombe wananchi muendelee kumuunga mkono Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli kwani ana upendo na wananchi,"alisema mwalimu Abdallah.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya Mika Likapakapa amempongeza mkuu wa wilaya,watumishi wa halmashauri kwa kusimamia shughuli za maendeleo katika wilaya nzima.