- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC JOKETI AAHIDI KUMPIGA JEKI DULA MBABE
SERIKALI ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani inatarajia kutoa eneo kwa ajili ya kujenga ukumbi utakaotumika kuwapatia mazoezi ya ngumi vijana wa wilaya hiyo.
Aidha imempongeza bondia Dulla Mbabe mzawa wa wilaya ya Kisarawe kwa ushindi alioupata dhidi ya mpinzani wake Fransis Cheka lillilofanyika hivi karibuni.
Hatua hiyo ya kupatiwa eneo hilo imetokana na bondia huyo kutoa kauli ya kutaka kutoa mafunzo kwa vijana wa kisarawe ili waweze kujifunza mchezo huo. Akizungumza kuhusu mpango huo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema,Mbabe amewatendea haki kwa kushinda pambano lililofanyika Desemba 26 mwaka uliopita dhidi ya Cheka.
Jokate alieleza, Kisarawe imejaa vipaji sio tu mpira wa miguu bali katika michezo mbalimbali. Aliahidi serikali ya wilaya kumpa uahirikiano kuhakikisha kipaji chake kinakua na kuibua vijana wengine.
Nae bondia huyo Mbabe alijigamba kwa kasema amecheza mipambano zaidi ya 20 ikiwemo ya kimataifa. Hata hivyo aliwaahidi watanzania kufanya vizuri katika Mchezo wa kimataifa unaokuja ambao unatarajiwa kufanyika mwezi march mwaka huu.
Katika hatua nyingine mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Zainab Vullu, alimhakikishia bondia huyo, wabunge wa mkoa huo watamkaribisha Dodoma katika bunge ili kumtambulisha na kuitambulisha Kisarawe kuwa inawanamichezo lukuki sio tu wa mpira wa miguu bali na masumbwi