- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DC AMTUPA NDANI MKUU WA SHULE KUJIHUSISHA NA NGONO NA WANAFUNZI
Mwanza: Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoan Mwanza, Juma Sweda amemweka rumande mkuu wa shule moja ya sekondari mkoani humo, akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya mapenzi na wanafunzi shuleni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Sweda alisema ushirikiano kati ya wananchi, na jeshi la polisi na sungusungu iliwezesha kumnasa mwalimu huyo kwa kuweka mtengo.
Alisema mwalimu huyo kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi Misasi akisubiri uchunguzi ukamilike na hatua nyingine zitafuata.
Alisema mwalimu huyo alikamatwa na baadhi ya wazazi na kisha kumpigia simu ambapo alienda katika eneo hilo na kuondoka naye hadi polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazomkabili.
Ofisa Elimu Wilaya ya Misungwi, Diana Kuboja alisema wanalaani tabia ya mwalimu huyo na na kwamba wanataka hatua kali zichukuliwe kwani huo ni ukiukwaji wa haki na unyanyasaji na pia iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
“Kitendo kama hiki ni fedheha kubwa sana miongoni mwa jamii, hawa ni watoto wadogo ambao hata hatma ya maisha yao hawaitambui.”
“Mwalimu kushiriki mapenzi na mwanafunzi huo ni udhalilishaji wa hali ya juu, sisi kama wadau wa elimu tuna laani,” alisema.
Mmoja wa wazazi wa shule hiyo, Chrisantusi Madoho alisema vitendo vya walimu wa kiume kuwadhalilisha wanafunzi wa kike vimekuwa vingi lakini ushahidi unapindishwa na kumuomba mkuu wa wilaya kuchukua hatua stahili dhidi ya mtuhumiwa.