Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:38 pm

NEWS: DC AAGIZA KUCHAPWA VIBOKO WAVAAJI NGUO ZA UTUPU

Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Bi. Veronika Kesi ametoa amri ya kupewa adhabu ya kuchapwa viboko kwa vijana au mtu yeyote atakaye onekana kuvaa mavazi yasiyo na staha na yatakayo onesha viongo vya ndani katika jamii ya wakazi wa Makete.

Bi. Kesi ametoa agizo hilo alipo kuwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa kata za Iniho na Kipagalo ambapo amesema mavazi hayo sio maadili ya wakazi wa wilaya yake pamoja na Tanzania kwa Ujumla.

Bila kueleza idadi gani ya viboko itolewe kwa vijana wakiume wanaovaa suruali mlegezo (chini ya makalio) au wasichana kuvaa mavazi yanayobana au yanayoonesha maumbile yao au mavazi yanayochora miili yao wachapwe viboko tangu kutolewa kwa amri hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kata hizo.

''Nataka kuona vijana suruali zenu zinashuka kutokana na wallet kuwa nzito umefanya shughuli zako huko walleti imejaa hela ndio ina inashusha sio kushusha tu ni viboko nasisitiza ni viboko wakati sheria za adhabu zingine zikiendelea kutungwa huko kwenye kata''