Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:32 pm

NEWS: DAKTARI AMFANYIA UPASUAJI MJAMZITO AKIWA AMELEWA CHAKALI

Taarifa kutoka nchini India zimeripoti kuwa Daktari mmoja jiana PJ Lakhani kutoka jimbo la Gujarat amekamatwa na polisi baada ya kumfanyia upasuaji mama mjamzito Kamini Chachi akiwa amelewa chakari.

Kwamujibu wa Maafisa wa Polisi nchini India wamesema kuwa mtoto alifariki muda mfupi tu baada ya upasuaji kufayika na mama akafuatia baada ya muda mfupi.

Baada ya tukio hilo Kipimo cha pumzi ya mdomo baadae kilithibitisha kuwa daktari aliyefanya upasuaji alikuwa amelewa

Daktari PJ Lakhani ni tabibu mwandamizi mwenye uzoefu wa kutosha na amekuwa akihudumu kwenye hospitali ya serikali ya Sonavala kwa miaka 15.

Mjamzito, Kamini Chachi, alipelekwa hospitali siku ya Jumatatu baada ya kupata uchungu.

Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa familia yake ambayo ilikuwa inasubiria habari njema iliarifiwa kuwa mtoto amefariki, na mama alikuwa akivuja damu sana.

Familia hiyo iliamua kumhamishia katika hospitali binafsi, lakini hakufika, alifia njiani.

Polisi pia imesema kuwa Dkt Lakhani aliwapigia simu kuwaomba msaada kutokana na hofu kuwa familia ya marehemu ingemshambulia mara baada ya vifo hivyo kutokea. "Tulimkuta akiwa amelewa, ndio maana tukamkamata," amesema ofisa wa polisi HR Goswami.