Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:48 pm

NEWS: CWT CHATAKIWA KUIFANYIA KAZI RIPOTI YA CAG.

JIJINI DOM: Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira Vijana Na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amekitaka Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kuifanyia kazi ripoti ya Mdhibiti na Mkagunzi Mkuu wa hesabu ya Mwaka Wa Fedha 2016/17 za Serikali ikiwemo kusimamia Suala nzima la matumizi bora ya fedha.

Mhagama ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati Akizungumza Na Wajumbe Wa CWT Katika Mkutano Maalum Wa Kujadili Ripoti Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali

Mbali na hayo amekitaka Chama hicho kusimamia na kuweka wazi Mikataba yote ya miradi ya Uwekezaji na vitega uchumi kwa uhalisia wake pamoja na kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wanachama wake.

Pia Mhagama ameagiza Uongozi Wa Chama hicho Kujiweka Utamaduni Wa Kuwajibika na Kusimamia Vyema Miradi ya Chama Kwa Manufaa Ya Wanachama.

Kwa upande wake rais Wa Chama Cha Walimu Nchini Mwalimu Leah Ulaya amesema Chama Kimejipanga Katika Kuhakikisha Kinasimamia Miradi Yote Ya Chama pamoja na Mikataba Yote iliyoingia kati Ya Chama na Wawekezaji Ikiwemo Vitega Uchumi Vilivyopo Katika Maeneo Mbalimbali Nchini.

Naye Rais Wa Shirikisho La Vyama Vya Wafanyakazi Nchini TUCTA Tumaini Nyamhokya amelitaka Shirikisho Kuhakikisha linawatumikia Wanachama Wake Kwa Uwazi na Uwajibikaji na kuahidi Kuwa TUCTA itaendelea Kutoa Ushirikiano Kwa Lengo La Kuboresha Maslahi Kwa Watumishi.