Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:31 am

NEWS: CUF YA LIPUMBA YATISHIA KUMUWEKA NDANI MAALIM SEIF

Mbunge wa jimbo la Kaliua wa chama cha wananchi CUF, Magdalena Sakaya amesema watamkamata kupitia Jeshi la polisi Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi iwapo atajaribu kufika katika jimbo la Liwale kwa nia ya kumnadi mgombea wa CUF bila kufuata utaratibu kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini.


Kauli hii inakuja ikiwa ni siku chache tangu Maalim Seif atangaze mpango wa kwenda kumnadi Mgombea wa jimbo la Liwale, Mohamed Mtesa ambaye alipitishwa na upande wa Profesa Lipumba. Ambapo licha ya pande hizo zote kuwa na migogoro zimenonesha kumuunga mkono mgombea huyo.
Sakaya amesema “Maalim Seif itakuwa ngumu kuingia Liwale, kwa sababu baada ya kukihujumu chama kwa muda mrefu tulitoa taarifa kwamba popote atakapofika akamatwe kwa sababu atahujumu tena, Makamanda wa mikoa na vituo vyote vya polisi Tanzania bara wanataarifa, akilazimisha kupanda jukwaa la kampeni atakumbana na nguvu ya Dola ".

“Sisi tulishawajua wao ni wahujumu siku zote, wamekuja kutuunga mkono kwa sababu CHADEMA wamejitoa kwenye uchaguzi, kwa hiyo tulikuwa tumeshawaandaa askari wetu ili wakionesha njama ya kutuhujumu wakamatwe, akitaka kuja kufunga kampeni lazima afuate taratibu, afike ofisini ili apangiwe na Mwenyekiti.” Ameongeza Sakaya
Kupitia Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF upande wa Maalim Seif, Mbarara Maharagande hivi karibuni alisema,

“Sisi upande wetu hatuna tatizo, kwa sababu yule ni Mwenyekiti wetu wa Halmashauri na viongozi wetu wameshaelekea huko kumuunga mkono, Maalim Seif wiki hii anatarajia kwenda kufunga kampeni, Sisi ndio tulimwambia akachukue fomu na apitishe kwa upande wa Lipumba kwa sababu ndie anayetambuliwa na dola ".