- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CPJ CHAMTAKA RAIS MAGUFULI KUWACHUKULIA HATUA MAAFISA UHAMIAJI
"Ni matarajio yetu kuwa, kama sisi, tumeumizwa na vitendo hivi ambavyo ni kinyume cha weledi wa kikazi; tabia ya unyanyasaji, na wewe utaweza kuagiza uchunguzi ufanyike na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na hili," CPJ imeeleza.
"Pia tumeshutshwa sana kwa taarifa kuwa waandishi waliokuwa wamekutana na timu yetu wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo kubwa na vitisho. Tunakuhimiza kuhakikisha kuwa waandishi wa Tanzania hawalengwi kwa sababu ya kazi yao," imeongeza.
CPJ inamtaka Magufuli kuwajulisha juu ya jawabu la serikali yake juu ya hili. "Tutakuwa tunafuatilia kupitia wawakilishi wa ubalozi wa nchi yako, imehitimisha barua hiyo."
Barua hiyo ilioandikwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ, Joel Simon, imeeleza kuwa Angela Quintal, anaye ongoza programu ya CPJ Afrika na Muthoki Mumo, mwakilishi wa CPJ katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara, walisafiri kwenda Tanzania Octoba 31 wakiwa na nia ya kuendelea na ziara yao mpaka Novemba 10.
Ameandika kuwa Lengo la wafanyakazi hao ilikuwa ni kuwatembelea waandishi wa habari wa Tanzania na taasisi za jumuiya za kiraia ili kupata uelewa zaidi juu ya uhuru wa habari katika nchi yako rais.
Kadhalika walikuwa wamealikwa na Baraza la Habari la Tanzania (MCT). Kabla ya kusafiri kuja Tanzania, walizungumza na wawakilishi wa serikali yako ambao waliwafahamisaha kuwa visa zilikuwa hazihitajiki kwa kuwa walikuwa wamepanga kufanya mikutano binafsi.
Mkurugenzi Mtendaji huyo ameeleza kuwa Quintal, raia wa Afrika Kusini, na Mumo, Mkenya walikuwa wameeleza nia yao wakiwa katika forodha ya Dar es Salaam, waliruhusiwa kuingia bila tatizo lolote, na walikuwa wakifanya shughuli zao waziwazi. Kwa bahati mbaya ziara yao ilisitishwa ghafla na maafisa waliowakabili kutoka serikali yako.
Jioni ya Novemba 7, maafisa wa serikali wakiwa katika nguo za kiraia ambao walijitambulisha kuwa ni maafisa wa uhamiaji walifika na kuingia ndani ya vyumba vya Quintal na Mumo hotelini, wakapekuwa vitu vyao na kuwalazimisha kuwa lazima waende wakahojiwe.
"Timu hiyo ya CPJ ilipandishwa kwenye gari kwa mabavu na madirisha kuwa yamefunikwa, na kupelekwa katika eneo lisilojulikana na wakawa wanahojiwa," CPJ imesema.