- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CONGO YAENDELEA ZUIA HUDUMA YA INTANETI NA MITANDAO YA KIJAMII
Hali ya sintofahamu bado inaendelea katika baadhi ya maeneo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya Huduma ya intaneti na mitandao ya kijamii kufungwa katika miji mbalimbali nchini humo, na hii ni siku moja tu baada ya uchaguzi mkuu wa Urais uliofanyika Jumapili Desemba 30.
Upinzani unashtumu serikali kutoa uamuzi wa kufungwa kwa huduma ya intaneti na mitandao ya kijamii ili kukataa aibu ya kushindwa kwa mgombea wa muungano wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary.
Hata hivyo zoezi la kuhesabu kura linaendelea, huku katika mji wa Goma, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa nchi zoezi hilo limemalizika tangu jumatatu jioni.
Wawakilishi wa Vodacom pia wamesema kuwa serikali iliwaagiza kufunga mawasiliano ya intaneti, kwa mujibu wa shirika la Habari la AFP. Lakini Waziri wa mawasiliano nchini humo Emery Okundji amesema kuwa hajui kuhusu hali hiyo.
Wagombea wakuu wa upinzani ni Martin Fayulu na Felix Tshisekedi.