- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CIA YASEMA MWANAMFALME WA SAUDIA NDIYO ALIYEPANGA MAUWAJI YA KHASHOGGI
Kitengo cha Intelejensia cha Marekani (CIA) Kimedhibitisha kuwa Mtoto wa Kifalme, wa Saud Arabia Mohammed bin Salman ndio aliagiza mauaji ya Mwanahabari, Raia wa Saudia Jamal Khashoggi katika Ubalozi mdogo wa nchi hiyo nchini Uturuki mwezi Octoba mwaka huu.
CIA imesema timu ya watu 15 ilienda Istanbul kwa kutumia ndege ya Serikali ya Saudia mwezi Oktoba na kumuua Khashoggi ndani ya Ubalozi wao alikoenda kuchukua nyaraka muhimu kwa ajili ya harusi yake na Mwanamke wa Kituruki
Ili kufikia hitimisho hilo CIA imedai kuangalia vyanzo mbalimbali vya taarifa ikiwemo kuingilia simu kati ya Balozi wa Saudi nchini Marekani ambaye ni Kaka wa Mohammed bin Salman, Khalid bin Salman na Khashoggi.
Inadaiwa Khalid alimwambia Khashoggi aende kwenye ubalozi wao huko Istanbul kuchukua nyaraka hizo huku akimuhakikishia kuwa ni salama kufanya hivyo.
Haiko wazi kama Khalid alikuwa anajua kama Khashoggi atauawa ila baada ya kuongea na Mwanahabari huyo alipiga simu ambayo uelekeo wake ni aliko kaka yake, Kiongozi wa Saudi Arabia
Hata hivyo, Msemaji wa Balozi ya Saudi iliyopo Washngton, Fatimah Baeshen amesema Balozi wake na Khashoggi hawakuzungumza chochote kuhusiana na kwenda Ubalozi wao